The Tanzanian civil society hosted a 2-day Tanzanian PreCOP27-conference to ensure that local voices, needs and stories are represented and amplified during the upcoming climate conference COP27 in Egypt. The upcoming COP27 in November has to be an African-focused climate conference that centres around African priorities and ad-dress urgently needed issues as Loss & Damage, Adaptation, Health and Climate Finance. Climate action need to be informed by bottom-up and on-field experience of vulnerable communities. The Pre-COP27 strengthened and em-powered African voices to focus African issues in-scope of COP27.
Learn in this Press Release on Swahili about the priorities of Tanzanian Civil Society for COP27.
MSIMAMO WA AZAKI NA WAWAKILISHI WA JAMII KUELEKEA MKUTANO WA KIMATAIFA WA 27 DHIDI YA MABADILIKO YA TABIANCHI WA UNFCCC.
Kila mwaka
nchi wanachama wa Umoja wa mataifa hukutana kujadiliana na kuweka mikakati
mbalimbali ya kudhibiti na kukabiliana na masuala mazima ya mabadiliko ya
tabianchi. Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa chini ya mwamvuli wa
mkutano wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi hushiriki mikutano hii
ikiwa na uwakilishi kutoka ofisi ya makamu wa raisi kitengo cha mazingira kama
wawakilishi wakuu wa nchi, wizara mbalimbali, na azaki
zinazofanya kazi katika uchechemuzi wa masuala ya mazingira, maliasili na mabadiliko ya tabianchi.
Mwaka huu,
mkutano huu unatarajiwa kufanyika Misri kuanzia tarehe 6/11/2022 mpaka 18/11/2022. Dhima kubwa ya mkutano huu ni kujadiliana ukamilishaji na
utekelezaji wa mkataba wa Paris wa kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa pia kuweka uwekezaji na utoaji wa pesa katika
nyezo/njia zinazo dhibiti uzalishaji wa gesi joto.
Tanzania
inautamaduni wa kukutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali kujadiliana na
kutengeneza msimamo moja ya nchi ambayo itaongoza wawakilishi wa Tanzania
katika mkutano huu wa majadiliano na kuhakikisha maslahi ya nchi yanazingatiwa
katika kuhakikisha uwezo na fursa za udhibiti na kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi. Mwaka huu azaki za CAN
Tanzania, FORUMCC, ActionAid, Save the Children na PINGOs
Forum kwa ufadhili wa Uk-Aid, FES Tanzania na Preston Werner Ventures,
wameandaa mkutano wa maandalizi kueleke mkutano mkubwa utakaofanyika Sharm
el Sheikh,Misri.
Mkutano huu umekutanisha wawakilishi wa azaki, vyama vya wafanyakazi,
vijana, watoto, wakulima, wafugaji, na wavuvi.
Hoja kubwa
ambayo wadau wanajadiliana na kutoa msimamo wa kuzingatiwa katika mkutano wa COP27
ni zifuatazo;
● Mchango wa Tanzania katika uzalishaji wa gesi joto ni mdogo sana, na jamii ya Tanzania inaathirika kwa kiwango kikubwa na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kipaumbele cha jamii ya Tanzania ni kwenye kuwezesha ustahimilivu wa athari za mabadiliko ya tabianchi na pamoja na kutoa ahueni ya hasara na uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
●
Tunasisitiza utoaji wa fedha
kuhakikisha uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kupata nafuu na ahueni kutokana na hasara na uharibifu unaosababishwa
na majanga yanayochagizwa na mabadiliko
ya tabianchi. Tunahitaji mifumo na michakato ya kuwezesha upatikanaji wa fedha
hizi kuwekwa vizuri na kuhakikisha upatikanaji wa moja kwa moja wa fedha hizi.
●
Tunasisitiza udhibiti wa uzalishaji wa gesi joto kwa nchi
zilizoendelea kwa kuongeza nia zao pamoja na kuwezesha ufyonzaji wa gesi joto,
ili kupunguza madhara na athari za mabadiliko ya tabianchi. uharibifu na upoteaji wa mali inayosababishwa na athari za
mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuhimiza ukamilishaji wa mkataba wa Paris.
●
Tunakataza ushawishi na uletaji wa nyenzo, teknolojia na
suluhisho zenye lebo ya ukabilianaji na athari za mabadiliko ya tabianchi
ambazo ni za uongo zisizo na tija katika utunzaji wa mazingira, zinazodidimiza
maendeleo na zinazo jenga utegemezi kwa nchi zinazoendelea.
●
Tunakataza siasa chafu zenye lengo la kuchelewesha
utekelezaji wa mkataba wa Paris na zenye kunufaisha wazalishaji wakubwa wa gesi
joto katika mkutano huu. Badala yake, tunasisitiza kuangalia zaidi masuala
yatakayo ongeza ustahimilivu na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi
●
Tunasisitiza uhitaji wa kujengewa uwezo na kupatiwa
teknolojia ili kuwezesha ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi pamoja na
kuwezesha hatua shahiki za kupunguza athari na uharibifu unaochagizwa na
mabadiliko ya tabianchi
●
Tunahitaji wawakilishi wetu kutoka Africa na kwenye makundi
ya pamoja kuwa na umoja na kusimamia hoja za msingi za maendeleo ambazo
zinazingatia uwezo na haja za jamii zilizo na mazingira magumu kustahimili
athari za mabadiliko ya tabianchi
●
Tunasikitishwa na upungufu wa kila mwaka wa uwakilishi na
ushiriki wa azaki na wawakilishi wa jamii katika Mikutano hii, kupitia utoaji
wa nafasi chache za ushiriki, uzuiaji wa kushiriki ndani ya vyumba vya mkutano
na vikwazo vingi kwenye utoaji visa kwa wenyeji wa mikutano. Tunahitaji nafasi
nyingi za uwakilishi kutoka kwenye jamii zetu ili kuhakikisha mslahi na
misimamo yetu inazingatiwa.